Mwanamke aliyejenga Miskiti 300 ukiwamo kichangani afariki dunia Abudhabi

Taifa la United Arab Emirates linaomboleza kifo cha Mama wa heshima katika Taifa hilo, Sheikhat Hassa Bint Muhammad Nahyan aliyefariki dunia mapema jana na kuzikwa jana hiyo hiyo mjini Abu Dhabi nchini humo.

Inaelezwa kuwa mama huyo amejenga misikiti zaidi ya 300 barani Afrika, ukiwemo msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni jijini Dar es salaam, nchini Tanzania, na hakuwahi kuiona 'Live' misikiti hiyo bali kwa kupelekewa picha tu.

Tayari Taifa hilo limetangaza siku tatu za maombolezo, huku bendera zake duniani kote zikipepea nusu mringoti, huku ikishindwa kuelezwa mara moja umri wa mama huyo.

Inna lilah wainna ilaih rajiun

Mungu ailaze roho ya mama Sheikhat Hassa mahala pema peponi.. Ameen.
 

Date: 
Monday, January 29, 2018 - 10:30